Wilibrodi (kwa Kiingereza cha Kale: Willibrord; kwa Kilatini: Villibrordus;[1] 658 hivi – 7 Novemba 739) alikuwa mmonaki Mbenedikto kutoka Northumbria (Uingereza) maarufu kama "Mtume wa Wafrisia" kwa uinjilishaji wake katika Uholanzi na Udeni za leo, alipoanzisha majimbo na monasteri mbalimbali[2].
Kwa kupewa daraja na Papa Sergio I alikuwa askofu wa kwanza wa Utrecht.
Kisha kuchoshwa na kazi na umri akafariki huko Echternach (leo nchini Luxembourg) katika monasteri mojawapo aliyoianzisha.[3]
Anaheshimiwa tangu zamani na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake[4].