Will Smith | |
---|---|
![]() Will Smith mnamo 2019 | |
Amezaliwa | Willard Christopher Smith, Jr. 25 Septemba 1968 Wynnefield, Philadelphia, Pennsylvania, West Philadelphia, Pennsylvania, U.S. |
Kazi yake | Mwigizaji, rapa, mtayarishaji wa filamu, mtayarishaji wa rekodi, mtayarishaji wa televisheni |
Miaka ya kazi | 1987–hadi leo |
Ndoa | Sheree Zampino (1992–1995) Jada Pinkett Smith (1997–hadi leo) |
Tovuti rasmi |
Willard Christopher "Will" Smith, Jr. (amezaliwa tar. 25 Septemba 1968)[1] ni mwigizaji, mtayarishaji wa filamu, na rapa kutoka nchini Marekani. Amefurahia sana mafanikio yake ya kimuziki, televisheni na filamu. Gazeti la "Newsweek" limemwita mwigizaji mwenye uwezo mkubwa kabisa duniani.[2] Smith amewahi kushindanishwa kwenye tuzo za Golden Globe mara nne, Academy Awards mara mbili, na ameshinda matuzo kede-kede ya Grammys.
Smith ameanza kujibebea umaarufu akiwa kama rapa chini ya jina la The Fresh Prince mwishoni mwa miaka ua 1980 na jina la uhusika kwenye mfululizo wa televisheni wa The Fresh Prince of Bel-Air. Filamu maarufu ambazo kacheza ni pamoja na Bad Boys na mfululizo wake wa pili Bad Boys II; Men in Black na mfululizo wake wa pili Men in Black II; Independence Day; I, Robot ; Ali; The Pursuit of Happyness; I Am Legend; Hancock; na Seven Pounds. Yeye ni mwigizaji pekee katika historia kuwa na mfululizo wa filamu nane zilizopata mauzo ya dola za Kimarekani milioni 100 kwenye sanduku la ofisi la nyumbani na vilevile kuwa kama mwigizaji pekee kuwa na filamu nane mfululizo kushika nafasi ya kwanza kwenye siku ya uzinduzi wa nyumbani akiwa kama mwigizaji kiongozi.[3]
{{cite web}}
: Unknown parameter |=
ignored (help)