William Courtet, O.P. (Serignan, 1590 – 29 Septemba 1637) alikuwa padri mmisionari kutoka Ufaransa na mmojawapo kati ya Wakristo wa Kanisa Katoliki waliofia dini nchini Japani.
Baada ya kufungwa gerezani kwa ajili ya Kristo zaidi ya mwaka mzima, alisulubiwa akakatwa kichwa.
Anaheshimiwa kama mtakatifu pamoja na Lorenzo Ruiz na wenzao waliotangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa wenye heri tarehe 18 Februari 1981 halafu watakatifu tarehe 18 Oktoba 1987.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 28 Septemba[1].
Mbali ya Lorenzo Ruiz, waliouawa pamoja naye ni: Mikaeli wa Aozaraza, Vinsenti Shiwozuka na Lazaro wa Kyoto[2].