William Ruto

William Ruto

William Ruto, 2022

Aliingia ofisini 
13 Septemba 2022
Deputy Rigathi Gachagua (2022–2024)
Kithure Kindiki (2024–)
mtangulizi Uhuru Kenyatta

Muda wa Utawala
9 Aprili 2013 – 13 Septemba 2022
Rais Uhuru Kenyatta
mtangulizi Kalonzo Musyoka
aliyemfuata Rigathi Gachagua

Waziri wa Elimu ya Juu
Muda wa Utawala
21 Aprili 2010 – 19 Oktoba 2010
Rais Mwai Kibaki
Waziri Mkuu Raila Odinga
mtangulizi Sally Kosgei
aliyemfuata Hellen Jepkemoi Sambili (kaimu)

Waziri wa Kilimo
Muda wa Utawala
17 Aprili 2008 – 21 Aprili 2010
Rais Mwai Kibaki
Waziri Mkuu Raila Odinga
mtangulizi Kipruto Arap Kirwa
aliyemfuata Sally Kosgei

Waziri wa Mambo ya Ndani
Muda wa Utawala
30 Agosti 2002 – Desemba 2002
Rais Daniel arap Moi
mtangulizi George Saitoti
aliyemfuata Moody Awori

Muda wa Utawala
29 Desemba 1997 – 9 Aprili 2013
mtangulizi Reuben Chesire
aliyemfuata (mbunge wa mwisho)

tarehe ya kuzaliwa 21 Januari 1967 (1967-01-21) (umri 57)
Kamagut, Kenya
chama UDA (2021–)
chamakingine
ndoa Rachel Chebet (m. 1991–present) «start: (1991)»"Marriage: Rachel Chebet to William Ruto" Location: (linkback://sw.wikipedia.orgview_html.php?sq=&lang=sw&q=William_Ruto)
watoto 7, ikijumuisha Charlene
makazi Ikulu
signature

William Kipchirchir Samoei arap Ruto (alizaliwa Kamagut, wilaya ya Uasin Gishu, 21 Disemba 1966) ni mwanasiasa wa Kenya ambaye amekuwa rais wa tano wa nchi kuanzia tarehe 13 Septemba 2022.

Alikuwa Waziri wa Kilimo tangu Aprili 2008 akawa makamu wa rais tangu mwaka 2013 hadi 2022.

Ruto aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Kenya African National Union, chama cha siasa kilichotawala zamani. Pia, alikuwa mbunge wa Eldoret Kaskazini tangu mwaka wa 1997, akawa Waziri wa Mambo ya Ndani mnamo Agosti 2002 lakini alipoteza nafasi hiyo baada ya uchaguzi wa Desemba 2002, ambapo KANU ilipoteza kwa muungano wa NARC.

Baada ya uchaguzi wa Kenya ya tarehe 9 Agosti 2022 Ruto alitangazwa kuwa mshindi tarehe 15 Agosti 2022. Matokeo yaliyotangazwa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na mipaka nchini Kenya Wafula Chebukati yalikanushwa na makamishna 4 wa Tume Huru ya Uchaguzi. Mpinzani wake Raila Amolo Odinga alikataa matokeo hayo na kuwasilisha kesi kwenye mahakama ya juu ya Kenya. Hata hivyo uamuzi ulithibitisha uhalali wa matokeo yaliyotangazwa awali.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne