Wimbo/nyimbo ni tungo zenye kufuata mapigo fulani ya kimi za kiafuziki yenye mahadhi ya kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti (urari wa sauti) na mpangilio maalumu wa maneno.
Nyimbo huundwa kwa lugha ya mkato na matumizi ya lugha ya picha (taswira).
Muundo wa nyimbo huwa ni wa kuimbika na mizani ya kila mstari mara nyingi huwa inalingana.
Wahusika wa nyimbo huwa ni mtu mmoja au kikundi cha watu. Nyimbo aghalabu huambatana na ala za muziki kama vile ngoma, zeze, marimba, makofi, vigelegele na kadhalika.
Mashairi ya nyimbo huimbwa popote pale panapostahili kulingana na tukio au muktadha unaofungamana na wimbo. Hivyo basi kuna nyimbo za dini, harusi, siasa, jando/unyago, kilimo, nyimbo za kuwinda na kadhalika.