Wimbo wa Taifa kwa kawaida ni wimbo (wakati mwingine pia musiki maalumu bila uimbaji) ulioteuliwa na serikali au kwa njia ya sheria na kutumiwa wakati wa nafasi maalumu kama alama au ishara ya taifa, nchi dola na kadhalika. Matumizi yake mara nyingi hufanana na matumizi ya bendera la taifa.
Nyimbo za taifa zilianza kuwa kawaida katika karne ya 19 katika madola ya Ulaya zikaenea polepole kote duniani pamoja na wazo la "utaifa".