Wistani

Mahali alipowahi kuzikwa.

Wistani (pia Wigstan, Wystan; alifariki Lichester, 840 hivi) alikuwa mfalme wa Mercia, leo nchini Uingereza ambaye alipinga ndoa ya malkia, mama yake, na ndugu wa karibu, ambaye alimuua kwa sababu hiyo [1][2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Juni[3].

  1. Wasyliw, Patricia Healy. Martyrdom, Murder, and Magic: Child Saints and Their Cults in Medieval Europe, Peter Lang, 2008, p. 78ISBN 9780820427645
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/92669
  3. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne