“With You” | |||||
---|---|---|---|---|---|
![]() | |||||
Single ya Chris Brown kutoka katika albamu ya Exclusive | |||||
Imetolewa | Marekani 4 Desemba 2007 Uingereza 24 Machi 2008 | ||||
Muundo | CD | ||||
Imerekodiwa | 2007 Battery Studios (New York City, New York) | ||||
Aina | Pop/R&B | ||||
Urefu | 4:11 | ||||
Studio | Jive, Zomba | ||||
Mtunzi | Johntá Austin, Tor Erik Hermansen, Mikkel Eriksen, Espen Lind, Amund Bjørklund | ||||
Mtayarishaji | Stargate | ||||
Mwenendo wa single za Chris Brown | |||||
| |||||
Kasha badala | |||||
![]() Kasha ya Australia, Ufaransa na Ufalme wa Muungano |
"With You" ni wimbo wa pop na R&B ya mwanamuziki Chris Brown, imetungwa na Johntá Austin, Tor Erik Hermansen, Mikkel Eriksen, Espen Lind na mwisho kabisa Amund Bjørklund.
Wimbo ulitayarishwa na Bw. Stargate ambaye pia alitayarisha wimbo wa "Unfaithful" na "Hate That I Love You" ya Rihanna na "Irreplaceable" ya Beyonce Knowles. Wimbo umetoka ukiwa kama single ya tatu kutoka katika albamu ya pili ya Brown ijulikanayo kwa jina la Exclusive ya mwaka wa 2007.
Wapenzi wengi wa muziki walikuwa wakiponda wimbo huu kwa madai ya kwamba eti unafanana sana na ule wimbo wa Beyonce (Irreplaceable), ingawaje Chris na Stargate hawajapata pigo lolote juu ya wimbo huu.
Kufuatia kutofanya vizuri katika chati wimbo wake wa "Wall To Wall" na "Kiss Kiss", "With You" ikatoka mnamo tar. 4 Desemba 2007 katika albamu zake za Marekani, na ikawa wimbo wake wa pili kupata mafanikio katika soko la muziki la kimataifa.