Yangeyange | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Yangeyange (Bubulcus ibis)
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 4:
|
Yangeyange ni ndege wakubwa wa jenasi mbalimbali ya nusufamilia Ardeinae katika familia Ardeidae wenye miguu mirefu, shingo ndefu na domo refu na jembamba. Hupinda shingo yao wakiruka angani. Ndege hawa ni weupe au weusi au rangi hizi mbili (pengine kijani au buluu). Spishi nyingine huitwa kulasitara au dandala. Yangeyange wengine hupenda kula samaki, wengine hula wadudu na wanyama wadogo kama vyura, mijusi na panya. Hujenga matago yao kwa matawi juu ya miti, mitete au mafunjo.