Sehemu ya mfululizo kuhusu |
Ukristo |
---|
|
|
Yesu (kwa Kiebrania יֵשׁוּעַ, Yeshua, kifupisho cha יהושע, Yehoshua, yaani "Mungu anaokoa") alikuwa Myahudi mwanamume aliyeishi miaka 2000 hivi iliyopita (labda 6 KK - 30 BK).
Alizaliwa na bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, huko Bethlehemu ya Uyahudi. Maisha yake yalikuwa ya pekee kwa kuwa alifahamu vitu vingi kwa mfano: sheria hata kuwazidi walimu wa sheria japokuwa hakusomea sheria. Alifanya pia maajabu mengi.
Ndiyo maana leo hii zaidi ya nusu ya wanadamu wote wanamuamini kuwa Mwana wa Mungu (ndio wanaoitwa Wakristo) au walau nabii (hasa Waislamu).
Kutokana na umuhimu wake katika historia ya binadamu, kwa kawaida miaka yote inahesabiwa kuanzia ujio wake (ulivyokadiriwa na Denis Mdogo kimakosa katika karne ya 6).