John Kemble (St Weonards, 1599 - Hereford 22 Agosti 1679) alikuwa padri Mkatoliki aliyefanya uchungaji kwa siri huko Uingereza kwa muda wa miaka 50 na zaidi[1].
Hatimaye alifia imani yake kutokana na dhuluma ya mfalme Charles II.
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini. Kwanza alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI mwaka 1929, halafu mtakatifu na Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970.