Yohane Mbatizaji wa Rossi (kwa Kiitalia: Giovanni Battista de' Rossi; Voltaggio, Piemonte, 22 Februari 1698 – Roma, Lazio, 23 Mei 1764) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki nchini Italia.
Papa Pius IX alimtangaza mwenye heri tarehe 13 Mei 1860, halafu Papa Leo XIII akamtangaza mtakatifu tarehe 8 Desemba 1881[1].
Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake[2].