Yohane Krisostomo

Yohane Krisostomo (karne XI.
Yohane Krisostomo na Gregori wa Nazianzo katika picha ya Kirusi ya karne XVIII.

Yohane Krisostomo, kwa Kigiriki χρυσόστομος, khrysóstomos, yaani «Mdomo wa dhahabu» alivyoitwa kutokana na ubora wa mahubiri yake, (Antiokia wa Siria, leo Antakya, nchini Uturuki, 347 hivi - Comana Pontica, Uturuki, 14 Septemba 407) alikuwa Patriarki wa Konstantinopoli, alipojulikana kama mchungaji mwema na mwalimu wa imani.

Ari yake ilisababisha apendwe na vilevile achukiwe sana. Hatimaye alifukuzwa na Kaisari ila Papa Inosenti I aliagiza arudishwe. Katika safari hiyo alinyanyaswa sana na askari walinzi wake akafa uhamishoni[1].

Tangu zamani anaheshimiwa kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Mwaka 1568 Papa Pius V alimuongezea sifa ya mwalimu wa Kanisa.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Septemba[2].

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/24400
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne