Yudea

Pompeus ndani ya Hekalu la Yerusalemu, kadiri ya Jean Fouquet.

Yudea (kwa Kilatini IVDAEA, kwa Kiebrania יהודה, Yehûḏāh au Yehuda, kwa Kigiriki Ἰουδαία) ni jina la jimbo la Dola la Roma kuanzia mwaka 6 hadi 135 BK.

Iliunganisha Uyahudi wenyewe, Samaria na Idumea chini ya liwali.

Asili ya jina ni kabila la Yuda, ambalo kuanzia karne ya 8 KK lilibaki karibu peke yake kati ya makabila 12 ya Israeli.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne