Yusti na Pastori (walifariki Alcalá de Henares, Hispania, 304 hivi) walikuwa wanafunzi wa shule Wakristo waliouawa kwa kukatwa kichwa katiaka dhuluma ya kaisari Dioklesyano [1]
Waliposikia gavana amefika ili kuua Wakristo, waliacha shuleni vifaa vyao vya kuandikia, wakakimbilia kifodini kwa hiari: mara walikamatwa, wakapigwa fimbo wakauawa huku wakifarijiana na kuhimizana.[2].
Inasemekana Yusti alikuwa na umri wa miaka 13, na mdogo wake Pastori chini ya miaka 9.
Mshairi Prudentius (348-410) aliwataja kwa majina.
Heshima ya watu kwao kama watakatifu wafiadini ni ya zamani sana.